[:en]*Written by Hawa Adinani and Amelia Hunt*

The meeting was conducted in two sub wards of Kigogo ward with participatory community discussions to see how community driven information can help to develop this plan.

Photo; Community meeting.

On the 26th and 27th of March 2018 the HOT Tanzania team conducted a pilot community meeting in Mbuyuni subward in Kigogo ward. The main objective of the meeting was to facilitate a discussion with different actors such as Mtaa Executive Officers  (MEO), Chairmen of the Subward, Councilors, Wajumbe leaders, Non Governmental Organizations and Community Based Organizations such as Tegemeo. Tegemeo provide education to the community on topics such as environmental education and how to support orphans – it operates nationwide.

During this meeting, community members pinpointed assets that they considered to be the most valuable within the Subwards and any possible threats to these assets perceived by the community. This information  allows Ramani Huria to produce a flood resilience plan. The maps will be the outputs produced after the information has been collected and organised using open source software.

Photo- Ward Leaders reading maps to identify their residences.

Community meetings were conducted with different key actors in the sub ward. Attendees included; Mtaa Executive Officers (MEO), Sub ward Chairmen, Councilors Wajumbe, Ten cells Shina Leaders, NGO and CBO partners (such as Tegemeo Wajumbe), government officials, private sector organisations, and religious leaders.

“I’m happy to be part of this, Knowing what is being done in my ward, participating in identifying safe and unsafe areas on a map can be a good start toward better planning” Mazoea Ling’omba- Mjumbe, Kigogo Kat subward.

The meeting was participated by 43 members from the two subwards, with participatory community meetings conducted in groups of 5 to 6 members. The exercise began by training participants how to read the map by identifying main features in the Subward and locating their area of residence. By the end of the group discussions participants were able to locate their houses and update street names on the map where information was missing or incorrect.

Photo; Maps are being updated by adding the missing information, risk areas are being identified  with the important asses in the ward.

“I’m proud to be part of this process – I have been trained  on how to read maps, and putting important things on a map to improve information for flood reduction” Miraji Simba- Red Cross Coordinator.

The most important lesson learnt from the workshop meeting is that it is the community members who are the key people needed to create a resilience plan. They are the ones who can identify historical flood trends and the location of key risk areas. (ie an engineer may be able to pinpoint flood risk areas based on calculations, but cannot provide the scope, history and impact of the flooding)- The information provided by community members allows a more accurate impression of the trend of flooding to be created with better understanding of how flood events have evolved over time.

Community members and Ward leaders were more reassured and excited about the project when they understood that the flood resilience plan was not intended to relocate people from their residence but rather to build a better plan on how to reduce flooding and suffering related to flooding.

“Initially my neighbors and I were a little worried that our houses may be demolished, but now we are at peace because the project was well explained to us. I will go and explain to ‘my people’ in the Shina to reassure them that the project is based on planning for resilience” Mjumbe- (Anonymous).

In these two Sub wards the main flood problems identified by community members were similar because the overall Ward is located between two major rivers, Msimbazi river and Kibangu river, that are ‘famous’ for causing flooding. It is clear that if the plans for flood resilience focus on accommodating people’s suggestions on the major community assets at risk and historical flood prone areas – improved mitigation plans can be produced which will reduce the effects of flooding.

 

 [:sw]Imeandikwa na Hawa Adinani na Amelia Hunt*

Mkutano ulifanyika kwenye mitaa miwili ya kata kigogo kama majaribio ili kuona ni jinsi gani taarifa za wanajamii zinaweza kuutumika kutengeneza mpango huu.

Picha; Mkutano na Wana jamii.

Tarehe 26 mwezi wa tatu 2018, Timu ya HOT Tanzania ilifanya mikutano ya majaribio kwenye mitaa ya Mbuyuni na Kigogo kati. Lengo kubwa la mkutano ilikuwa kuhamasisha majadiliano na wadau mbalimbali kama Mtendaji wa mtaa, Mwenyekiti wa mtaa Wajume, Asasi zisizo za kiserikali na mashirika ya kijamii kama Tegemeo. (Tegemeo ni shirika linalotoa elimu kwa jamii kwenye mambo ya elimu ya mazingira na kusaidia yatima- Inafanya kazi nchi nzima.

Kwenye mkutano huu, Wanajamii walionyesha maeneolvitu ambavyo wanaona vina thamani sana kwenye mitaa yao. Taarifa hizi zitawezesha Ramani Huria kutengeneza mpango wa kupambana na mafuriko. Ramani hizi zitakuwa ni zao lililotokana na taarifa zilizokusanywa wakati wa mkutano na kupangiliwa kwa kutumia programu ya huru kama QGIS.

Picha- Viongozi wa mtaa wanasoma ramani na kuonyesha makazi yao.

Ninafurahi kuwa sehemu ya zoezi, Kujua nini kinaendelea kwenye mtaa wangu, kushiriki kwenye kutambua maeneo salama na yasiyo salama kwa kutumia ramani ni mwanzo mruri ili kutengeneeza mpango wa kupambana na mafuriko” Mazoea Ling’omba- Mjumbe, Mtaa wa Kigogo Kati.

Mkutano ulihudhuriwa na washiriki 43 kutoka mitaa miwili, kwa mikutano shirikishi iliyo huisha makundi ya watu wanne hadi watano. Zoezi lilianza kwa kuwaelekeza washiriki jinsi ya kusoma ramani, kuonyesha maeneo muhimu na kuonyesha makazi yao. Mwisho wa majadiliano washiriki waliweza kuonyesha nyumba zao na kuongeza majina ya mitaa ambapo kulikuwa hakuna taarifa au hazikuwa sahihi.

Picha; Ramani zinaboreshwa kwa kuongeza taarifa zilizo kosekana, maeneo hatarishi yana onyeshwa kwa vitu muhimu kwenya mtaa..

“Najivunia kuwa sehemu ya mchakato huu- Nimepewa  mafunzo ya jinsi ya kusoma ramani, na kuweka vitu muhimu kwenye ramani kuboresha taarifa kwa ajili ya kupambana na mafuuriko” Miraji Simba- Mratibu Red Cross.

Somo muhimu lililo jifunzwa kutoka kwenye warsha hii ni kuwa wanajamii ndio watu muhimu katika kutengeneza mpango huu. Wao wanaweza kutoa historia na mwenendo wa mafuriko na kuonyesha maeneo yaliyo kwenye hatari ya kupata mafuriko ( Kwa mfano mhandisi angeweza kujua ni wapi kuna mafuriko kwa kutumia mahesabu, lakini hawezi kutoa wigo historia na athari halisi za mafuriko)- Taarifa walizotoa wanajamii zinaonyesha mwonekano halisi na mwenendo wa mafuriko na kutoa uelewa zaidi wa jinsi mafuriko yalivo badilika kulingana muda.

Wana jamii na viongozi wa kata walijihakikishia na walikuwa na furaha kuhusu mradi huu pale waliposikia kuwa mpango huu wa kupambana na mafuriko hauhusishi kuwahamisha kwenye makazi yao bali kutengeneza mpango mzuri wa jinsi ya kupunguza mafuriko na na mateso yatokanayo na athari za mafuuriko.

Mwanzoni mimi na jirani zangu tulipta wasiwasi kuwa nyumba zetu zitabomolewa, lakini sasa tuna amani kwa  kuwa mradi umeelezwa vizuri kwetu. Nitaenda kuwaelezea “watu wangu” kwenye shina ili kuwahakikishia kuwa mradi huu ni kwa ajili ya mpango wa kupambana na mafuriko na si kuvunja nyumba”Mjumbe- (jina limehifadhiwa).

Kwenye mitaa hii miwili, matatizo yote yaliyo onyeshwa na wana jamii yanafanana kwa sababu Kata nzima ya kigogo ipo kati ya mito miwili mikubwa- mto  Msimbazi na Kibangu ambayo ni mito “maarufu” inayosababisha mafuriko. Ni wazi kuwa mpango huu wa kuzuia mafuriko unalenga kwenye kuweka mapendekezo ya wana jamii ya vitu vya muhimu ambavyo vipo kwenye hatari ya kupata mafuriko na historia ya maeneo yanayopata mafuriko- Mpango ulioboreshwa wa kupunguza athari za mafuriko unaweza kutengenezwa.

 [:]